
Rais Jakaya Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais wa hovyo ambaye Tanzania haijawahi, na saa nyingine, hatawahi kupata. Hivi karibuni alimteua afisa usalama aliyetuhumiwa kumtesa Dk Steven Ulimboka, Jack Mugendi Zoka kuwa balozi nchini Kanada.Ni aibu namna gani kwa mhalifu kama huyu kupewa ubalozi? Kama haitoshi, juzi kamteua Paulo Makonda kuwa mkuu wa wilaya wakati anafahamika alivyomfanyia fujo jaji Joseph Warioba. Kama haitoshi aliongezea na uteuzi wa mtangazaji Shaaban Kisu wa TBC na afisa mwandamizi wa zamani wa jeshi la polisi Zelote Stephen kuwa wakuu wa wilaya licha ya manung'uniko mengi toka kwa wananchi kuhusiana na kutokuwa na sifa wala udhu kwa wateule hawa.