
Hapa ni ujumbe wa wazira ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukiwa kwenye matanuzi huko Singapore kwa kisingizio cha ziara ya kikazi. Kwanini ziara ya kikazi isifanyike nchini badala yake ifanyike ughaibuni kama siyo kutaka kutalii na kutafuta kulipwa per diem? Walianza wizara ya Utalii na sasa hawa wamefuatia. Kesho utaona ujumbe wa wizara nyingine nje ukitalii kwa kisingizio cha kujifunza hili na lile wakati ukweli hii ni aina mpya ya ufisadi. Nani atawazuia iwapo bosi wao mwenyewe Vasco da Gama JK ni bingwa wa jinai hii?