Kuna tabia ya ajabu imejitokeza ambapo baadhi ya watanzania wanaoishi nje ya nchi hujikomba kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama njia ya kurejerea nyumbani. Majiji ya Washington, New York na London yanaongoza kwa wasanii kujifanya wana uchungu na CCM. Jamani kama mmeshindwa si mrejee huko mkawa wakereketwa tu? Watu badala ya kujisomea na kutafuta maisha kwa njia halali wanaingia usanii kiasi cha kutia kinyaa. Pichani hapo juu mtoto wa rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani au rais wa nyuma ya pazia anawasili New York tayari kwa maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa CCM. Hawa wanaomwambudia Kikwete na ukoo wake makaratasi yao yamekaa sawa? Kama yamekaa sawa, wamejiandaa vya kutosha kuishi maisha ya mpambano huku ugenini? Wamejiongezea maarifa angalau wawe na cha kurejea nacho nyumbani kama wataamua? Au wameamua usanii na kujikomba kama mtaji? Mimi hakika sielewi.