




Hali ilivyo ni kwamba Blaise Compaore imla wa taifa maskini la Bukinabe amefikia arobaini yake. Compaore alichukua madaraka mwaka 1987 baada ya kumpindua na kumuua rafiki yake rais Thomas Sankara aliyependwa na kusifika kwa usafi na uzalendo wake. Wengi walishangaa na kulaani kitendo hiki cha kinyama na hovyo kufanywa kwa rafiki. Hivyo, wengi wangependa na wanangoja kwa hamu kuona mwisho wa muuaji na fisadi huyu anayetuhumiwa kutumia viungo vya mazeruzeru kutambikia ili aendelee kukaa madarakani. Long live Burkinabe, Long live Thomas Sankara's spirit working in the people of Burkinabe.