Japa nilipokea nakala ya kitabu juu ya marehemu Dk Sengondo Mvungi Breathing the Constitution toka Tanzania. Kilitumwa na Kituo cha Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre-LHRC). Kwa namna ya pekee nawashukuru LHRC kwa kunitumia nakala ya kitabu hichi ukiachia mbali kutumia moja ya makala zangu kwenye kitabu husika uk. 86. Namshukuru Dk Elen Kijo-Bisimba aliyehakikisha natumiwa nakala hii. Pia nimepata fursa ya kushiriki kwenye kueleza maisha ya nguli huyu wa sheria na haki za binadamu aliyeuawa kwenye mazingira ya kutatanisha kipindi alipohitajika kutoa mchango wake kwenye upatikanaji wa katiba safi ya wananchi ambayo hata hivyo imechakachuliwa na mafisadi ili kulinda uoza wao. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Dk Sengondo Mvungi. AAAMIN.
↧