Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175

Swali la leo: Iweje Faru na Tembo wauawe Bongo kampeni London?

$
0
0
Ivory destruction
Pesa ya wizi, ufisadi, rushwa, unga na ujangili wanaficha London.
Safari za kikazi wanafanya London.
Kampeni ya uzazi wa mpango London.
Mikutano ya uwazi London'
Kampeni ya kuangamiza ujangili London.
Je ni kwa nini au ni kwa vile hawa jamaa ndiyo waliotutawala?
Je ni roho kuwasuta wahusika ambao walirithi faru na tembo kibao toka kwa wakoloni?
Wakoloni walikuja wakatuibia lakini walikuwa na akili wakatubakishia.
Sisi tulipopata uhuru ambao umegeuka udhuru tumejitahidi kujiibia na kumaliza kana kwamba hakuna vizazi vijavyo. Sijui ndiyo huu uvivu wa kufikiri au kufikiri kivivu! Sijui ndiyo huko kuishiwa au sanaa za kuwaweka sawa wafadhili majangili ya ofisini na mbugani yakaendelea kupeta?
Nukuu ya leo ni toka kwa Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA).
Alikaririwa hivi karibuni akihoji,“Inakuwaje mtu anayevunja sheria za nchi hakamatwi. Waziri Nyalandu amekuwa mlalamikaji badala ya kutafuta suluhu, majibu yake na ya Serikali ya CCM yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaogopwa unaihusisha Ikulu, wanasiasa, polisi, maofisa wanyamapori na wanajeshi.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175