
Usiku wa kuamkia tarehe 16 Desemba hii ulishuhudia mapigano makali baina ya vikosi vya jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vile vinavyoaminika kumtii makamu wa rais wa zamani Dk Riek Machar aliyetimuliwa hivi karibuni na rais Salva Kiir Mayardit.
Inasikitisha kwa nchi changa kuliko zote duniani kuanza kuadamwa na jinamizi la uporaji wa madaraka unaotakana na hisia za kikabila na tamaa ya madaraka. Je mamlaka mjini Juba zitashughulikiaje kitisho hiki bila kukiuka haki za binadamu? Je kuna mkono wa mtu hasa Sudan Kaskazini ambayo imekuwa ikituhumiwa kuwaunga mkono waasi wanaopigana na serikali ya Juba yenye utajiri wa mafuta? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.