
Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel ametoa mpya kwa kurejea darasani kufundisha historia ya taifa lake. Wakati wa maadhimisho ya 52 ya kujengwa kwa ukuta wa Berlin ambao kuangushwa kwake kulimaliza vita baridi kati ya kambi za Magharibi na Mashariki, Merkel aliwaacha hoi wajerumani alipoamua kurejea darasani kufundisha historia. Merkel ambaye ana shahada ya uzamivu katika Fizikia aliyeandika karatasi nyingi za kisomi, aliamua kufundisha somo la historia. Je ni viongozi wangapi wa kiswahili wanaweza kurejea darasani kufundisha? Hebu piga picha marais kama Jakaya Kikwete, Jacob Zuma, Joseph Kabila, Paul Kagame,Yahya Jammeh, Uhuru Kenyatta na wengine wenye elimu za kuokoteza. Hakika bado Afrika ina ukame wa viongozi! Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.