Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178

Ziara za siri za Kikwete zina manufaa kwa taifa?


Image may be NSFW.
Clik here to view.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakipigiwa nyimbo za mataifa hayo mawili kabla ya kukagua gwaride rasmi mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei, 5, 2013. 

 Rais Jakaya Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais wa hovyo na dhaifu ambaye Tanzania imewahi kupata. Inakuwaje rais wa nchi anafanya ziara tena nje ya nchi na umma wa watanzania haufahamishwi? Nimeshangaa kusikia kuwa rais Kikwete yuko ziarani nchini Kuwait. Nimeshangaa kusikia kuwa rais ameondoka kimya kimya bila umma kujua kana kwamba anakwenda kule kuiwakilisha familia yake yake na si nchi.  Inashangaza kuona hata magazeti ya serikali hayajabeba habari hii!Hata tovuti ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliogopa kuchapisha habari hii hadi blog hii ilipolalamika wakabandika picha kama nusu saa baada ya kutoa lalamiko. Tunaipelekea wapi nchi yetu? Tumefikia mahali tunatawaliwa kihuni na kipuuzi hivi! Hii maana yake ni kwamba ziara hii ni ya shaka tupu. Je ziara za siri namna hii zina manufaa kwa taifa? Tukimuita Vasco da Gama wapambe na waramba viatu wake wanalalamika kuwa tunamkosea adabu. Tutamheshimuje mtu asituheshimu wala asiyeheshimu sheria wala taratibu? Tutamheshimuje mtu anayejitembeza kama changu akidhalilisha taifa letu? Tutamheshimu kwa lipi iwapo ameshindwa kulhali? Nani anaweza kumheshimu ombaomba anayetembea juu ya dhahabu akiomba ugolo? Ingawa juzi mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) profesa Ibrahim Lipumba aliwalaumu Benjamin Mkapa na Andrew Chenge kwa kuiuza nchi yetu kwa wawekezaji, Kikwete anaonekana kuendeleza upuuzi huu  kwa kiwango cha kutisha. Inakuwaje rais aende ziarani kwa kodi ya wananchi halafu wasifahamishwe? Hivi ikitokea akafia huko tutaelewana? Je Kikwete anaficha nini? Imefikia mahali rais wetu anafanya mambo kana kwamba anakwenda kuzini kutokana kuficha wajumbe anaoandamana nao? Blogu hii imelalamikia mchezo huu mchafu bila majibu. Hata hivyo, hatutaacha kupiga kelele. Hata wakinyamaza wanapata salamu zetu. Zinawaudhi na kuwatisha hata kama hawasemi. Kuna haja ya wajuzi wa mambo kufuatilia alichokwenda kufanya Kikwete Kuwait ambacho amekifanya siri. Anaweza kutuficha leo. Kesho tutajua. Maana akishaingia mikataba yake ya kijinga tutawaona hao wanaomhangaisha hadi anafanya vitu ambavyo hata hayawani hawezi kufanya mitaani kama siyo kwenye mbuga zetu. Nani mara hii kasahau kuwa waarabu wanaongoza kwenye kufanya ujangili uliohalalishwa na watawala mataahira wakikuwadiwa na Abdulrahaman Kinana katibu mkuu wa CCM? Nani amesahau kashfa ya Loliondo ambapo iliuzwa kwa mwarabu toka Oman ambaye ni rafiki na mshirika wa Rostam Aziz aitwaye Brig. Ali uliofanywa nwa Ali Hassan Mwinyi na mramba viatu wake Muhidin Ndolanga hadi kusababisha kifo cha Stan Katabalo alipofichua hujuma hii? Sitashangaa kusikia kuwa Kikwete amesaini mikataba ya kuruhusu Kuwait wawekeze kwenye kilimo cha kuzalisha chakula kwa ajili ya watu wao. Maana nchi nyingi za ghuba kutokana na utajiri wa mafuta zimeigeuza Afrika sehemu ya kuzalishia chakula cha watu wake wakati wenye nchi wanaishi ima kwa kutegemea misaada au kufa njaa. Ni aibu ya namna gani rais wetu kufanya vitu kama vile hatuna hata mtu mmoja mwenye akili wa kumshauri.
Hakika rais wetu ni ajali mbaya ya kihistoria ambaye madhara yake yatachukua mamia ya miaka kuondoka.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178

Trending Articles


Girasoles para colorear


mayabang Quotes, Torpe Quotes, tanga Quotes


Tagalog Quotes About Crush – Tagalog Love Quotes


OFW quotes : Pinoy Tagalog Quotes


Long Distance Relationship Tagalog Love Quotes


Tagalog Quotes To Move on and More Love Love Love Quotes


5 Tagalog Relationship Rules


Best Crush Tagalog Quotes And Sayings 2017


Re:Mutton Pies (lleechef)


FORECLOSURE OF REAL ESTATE MORTGAGE


Sapos para colorear


tagalog love Quotes – Tiwala Quotes


Break up Quotes Tagalog Love Quote – Broken Hearted Quotes Tagalog


Patama Quotes : Tagalog Inspirational Quotes


Pamatay na Banat and Mga Patama Love Quotes


Tagalog Long Distance Relationship Love Quotes


BARKADA TAGALOG QUOTES


“BAHAY KUBO HUGOT”


Vimeo 10.7.0 by Vimeo.com, Inc.


Vimeo 10.7.1 by Vimeo.com, Inc.