Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173

Hawa ni katika wachache waliobarikiwa na kuwahi kuishi

$
0
0
  • In this photo taken on Thursday, Feb. 26, 2015, Spring Valley resident Duranord Veillard and his wife Jeanne Veillard are photographed in Spring Valley, N.Y. Duranord Veillard celebrates his 108th birthday on Saturday, Feb. 28, 2015 and his wife, Jeanne will turn 105 in May. The Veillards have been married 82 years and are one of the oldest married couples in New York. (AP Photo/The Journal News, Tania Savayan) NYC OUT, NO SALES, ONLINE OUT, TV OUT, NEWSDAY INTERNET OUT; MAGS OUT
    Duranord Veillard (108) na Mkewe Jeanne Veillard, (105)

    Ni wakazi wa  Spring Valley New York licha ya kuwa na miaka mia na ushei wamedumu katika ndoa kwa jumla ya miaka  82. Je ni wangapi wanabahati kuishi miaka 82 ukiachia mbali kuishi katika ndoa kwa miaka hiyo? Nadhani kama kuna watu waliobarikiwa na ambao wanaweza kuonekana kama si wa kawaida si wengine bali Duranord na Jeanne. Tofauti na wenzao weupe wanaopelekwa kwenye majumba ya vikongwe na kufa huko kwa upweke, wanandoa hawa bado wanaishi na binti yao anayewatunza kama mila za kiafrika zilivyo. Wanandoa hawa waliobarikiwa walijaliwa kuwa na watoto watano. Baba alikuwa ni mtaalamu wa maabara hospitali. Kazi ya mama haikutajwa. Ila walihamia Marekani mwaka 1968. Pamoja na kutoona vizuri wawili hawa bado wanaweza kufanya utani na watu huku baba akiwa bado na uwezo wa kupiga push ups kila siku. Ni bahati mbaya hatukupata habari nyingi juu ya wawili hawa ambao ni katika wachache waliofanikiwa kuishi umri huu ukiachia mbali kuwa pamoja tena kwa miaka zaidi ya 80. Je ni bahati kiasi gani?

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173