“Watanzania tumejaa ubinafsi, kila mtu anafikiria kila anafanya jambo anategemea kupata posho, na niwahakikishieni mimi sina uchu wa ubinafsi wala tamaa za vyeo kwani kama ni cheo nilichoacha UN kilikuwa kikubwa zaidi,” Profesa Anna Kajumlo Tibaijuka. Hii nukuu imechukua nafasi ya kwanza kwa ubovu kwanza, kutokana na hadhi ya aliyeitoa kielimu. Na pili mjumlisho wake. Hivi huyu hakusoma kanuni na miiko ya uwasilishaji taarifa? Je hajui kuwa mjumlisho ni kiashiria kikubwa na cha juu cha ujinga? Inakuwaje profesa mzima anasema eti watanzania wote wana ubinafsi wakati yeye anayesema si mbinafsi ni mtanzania? Unawezaje kusema "kila mtanzania" utadhani umeongea na watanzania wote? Angalau angetoa hata takwimu lau kuficha ujinga na ujuha wake.![]()
“Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipoulizwa na Kamati ya Bunge alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL,” Rais Jakaya Kikwete. Je kama fedha ni za IPTL ni kwanini umekubali kujiuzulu kwa Mwanasheria mkuu wa serikali na kumtimua waziri wa zamani wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka kwa kukatiwa fedha hiyo hiyo ambayo si ya umma bali IPTL?
Hebu soma nukuu nyingine ya Kikwete ili uamue mwenyewe, “Tumezungumza na Profesa Tibaijuka na tumemuomba atupishe ili tuweze kuteua waziri mwingine kwani viashiri vyote vinaonyesha kuwa alikiuka kanuni na sheria ya maadili ya Umma.” Maadili gani ya umma yamekiukwa kwa kupokea fedha halali sawa na serikali inavyopokea misaada toka Ughaibuni?