Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173

Viongozi wa dini na kujikomba kwa rais

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akiwa pichani ikulu pamoja na baadhi ya viongozi wa dini waliokwenda kumuombea baada ya kurejea toka kwenye matibabu ya kansa ya kizazi huko Marekani. Inashangaza viongozi wetu wa kiroho wanavyojigonga kwa rais. Wanapataje muda wa kwenda eti "kumuombea" lakini wakashindwa kumwambia kuwa anatawala nchi kifisadi huku akihalalisha wizi wa fedha za umma? Hawa kweli ni viongozi wa dini au wajanja wanaotumia majoho kukidhi njaa zao? Je ni wagonjwa wangapi wanaoza mahospitali na hawa hawa wanaojitia viongozi wao wa kiroho hawaendi kuwaombea? Hawa wameenda kumuombea Kikwete au kumuomba awape chochote kitu? Viongozi wa dini wanapofunga ndoa na wanasiasa wachafu mjue taifa linaangamia.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173