
Je hiki kibonzo ni utani au ukweli? Ni mtanzania gani anaweza kusema hayuko hivi? Kama hauko hivi basi ndugu, majirani hata ndugu wa ndugu wa ndugu zako hata marafiki wa marafiki wa marafiki zako wako katika hali hii. Nawaona Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wakiwa wamevuaa manyang'unyang'u huku wakikalia mwamba wa almas. Je hapa tatizo ni akili au utashi? Je tatizo ni utaahira au upumbavu? Tatizo ni upofu au ugonjwa? Sijui tatizo ni nini kati ya uroho na roho mbayaTafakarini?