
Waziri wa Fedheha, sorry Fedha, Saada Mkuya akisaini mkataba wa makabidhiano ya shilingi bilioni 45 na mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudi Arabia Hassan al Attas jijini Dar. Inashangaza nchi inavyoomba omba na kukopa lakini bado ikaruhusu ufisadi wa kutisha kama vile wa escrow. Je hii misaada tunayopewa ni misaada au kuna mengine nyuma yake? Kwanini hawa wanaotoa misaada kama wana nia nzuri wasiulize hizi tunawamwagia mafisadi kwanza? Je wanatumia udhaifu wa utawala wetu kujipenyeza watuumize baadaye? Inakuwaje Saudia watoe msaada wa kifedha hata kabla ya wafadhili hawajatoa tamko kuhusiana na kashfa ya escrow iliyowafanya wagome kuchangia shilingi bilioni moja kwenye bajeti ya taifa? Je Saudia inaanza kupingana na wafadhili? Ili iweje? Maswali ni mengi kuliko majibu.