Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173

Hii nayo imekaa vipi?

$
0
0

Baada ya kunusurika kukumbwa na maji, JK atakuwa anachekelea ujinga na papara za bunge letu na upinzani kwa kushindwa kushughulikia serikali nzima wakaridhika na kafara ya vijidagaa. Uamuzi hafifu na wa aibu wa Bunge umethibitisha jinsi upinzani usivyo na mipango ya kuchukua nchi. Maana kama ungekuwa na visheni na mipango mikubwa, kwa kutumia msimamo wa wafadhili ungewataka wananchi waingie mitaani na kuiondoa serikali hii fisadi na dhalimu ya JK. Bahati mbaya, kwa upofu na upogo wao hawakuliona hili. Halafu bado wanajipiga vifua kuwa wamewashughulikia mafisadi wakati mkubwa wao akiendelea kupeta katika nchi hii iliyogeuzwa shamba la bibi chizi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173