Ukiwa na kasoro wengi wanaitumia kukugeuza kinyago hata mwanasesere. Wanakuchezesha kama kile kinyago cha Joyce Wowowo. Hivi Kikwete na uprofesa tena wa kilimo wapi na wapi? Je hawa kuna kitu wanachotaka kama vile kupewa ardhi wakalime chakula cha kulisha watu wetu. Je hii nayo si aina mpya ya rushwa? Kama hii si rushwa, mbona huo udaktari na uprofesa wa heshima hawapewi viongozi wa mataifa makubwa? Sijawahi kusika Obama kazawadiwa uprofesa wala Putin udaktari. Kuna haja ya kuwa na katiba inayozuia viongozi malimbukeni kuhongwa upuuzi kama huu. Kama unataka uprofesa au udaktari kasome.