![]() |
Wanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Kiwalani wakifanya mtihani wao wa kumaliza darasa la saba picha kwa hisani ya IPP media.
![]() |
Kwa watu walioingizwa mkenge kwa kuahidiwa `Maisha Bora kwa Wote (MBW) sijui wakishuhudia hali kama hii ambapo watoto wao wanafanyia mitahani yao sakafuni wanajisikiaje? Hapo juu mwanafunzi wa shule ya Msingi Kiwalani Jijini Dar akipokea nakala ya maswali ya ya mtihani wake wa kumaliza darasa la saba toka kwa msimamizi. Kweli huyu anaweza kushinda kuingia kidato cha kwanza? Je haya ndiyo Maisha Bora kwa Wote walioahidiwa au utapeli mtupu? Wakati upuuzi huu ukiendelea, aliyewaahidi yote haya anaruhusu Bunge Maalum la Katiba (BMK) kuendelea na vikao kinyume cha sheria na kuiba pesa ambayo angalau ingeweza kununuliwa madawati,Hivi hii pesa inayopotea ingeweza kusomesha watanzania wangapi na kupunguza ujinga kwa kiasi gani? Je ingeweza kutibia watanzania wangapi? Je ingeweza kujenga kilometa ngapi za barabara au kuleta lita ngapi za maji?