Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178

Kwa dada wa Kitanzania

$
0
0


Baada ya kusoma gazetini BOFYA HAPA kuwa dada wa kitanzania wanapelekwa China kuuza miili yao nilishawishika kuandika comment ifuatayo:Tamaa, ujinga, kutaka kuukata, umaskini na roho mbaya vinaponza watu wetu. Nashukuru mwandishi ameandika hili ingawa hata wakaposoma hawataamini hadi yawakute. Siku hizi kila mtu anataka kwenda ng'ambo hata bila mipango na taarifa sahihi. Wataumia wengi kama serikali yenyewe inaendeshwa na wasanii. Kimsingi, haya magenge ya kusafirisha binadamu yanashirikiana na viongozi wakubwa serikalini. Hii ni jinai sawa na madawa ya kulevya ambayo inalindwa na rais aliyekiri kuwa na majina ya vigogo wake asiwashughulikie. Dada zetu wanapaswa kutulia na kuanza kubuni mbinu halali za kuishi badala ya kujidanganya na kudanganywa kuwa ughaibuni ndiyo kuna maisha. Kwenda ughaibuni si kosa iwapo utafanya hivyo kwa njia halali na zinazowezekana na kueleweka badala ya kukubali kila ahadi za kipuuzi. Hilo moja. Kuna waganga wa kienyeji na wachungaji uchwara wanaotajirika na kuharibu maisha ya wanawake wengi kwa kuwahadaa kuwa wanaweza kuwafanikishia wanachotaka. Mtadhalilishwa, kunyonywa, kudhulumiwa hata kuuawa kwa tamaa na ujinga wenu. Tieni akilini. Kama mambo yamekushindwa kwenu utayaweza ugenini?

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178

Trending Articles


Girasoles para colorear


mayabang Quotes, Torpe Quotes, tanga Quotes


Tagalog Quotes About Crush – Tagalog Love Quotes


OFW quotes : Pinoy Tagalog Quotes


Long Distance Relationship Tagalog Love Quotes


Tagalog Quotes To Move on and More Love Love Love Quotes


5 Tagalog Relationship Rules


Best Crush Tagalog Quotes And Sayings 2017


Re:Mutton Pies (lleechef)


FORECLOSURE OF REAL ESTATE MORTGAGE


Sapos para colorear


tagalog love Quotes – Tiwala Quotes


Break up Quotes Tagalog Love Quote – Broken Hearted Quotes Tagalog


Patama Quotes : Tagalog Inspirational Quotes


Pamatay na Banat and Mga Patama Love Quotes


Tagalog Long Distance Relationship Love Quotes


BARKADA TAGALOG QUOTES


“BAHAY KUBO HUGOT”


Vimeo 10.7.0 by Vimeo.com, Inc.


Vimeo 10.7.1 by Vimeo.com, Inc.