Hapa chini ni makazi ya kifahari ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye ameapishwa leo kwa kipindi kingine cha pili na cha mwisho kama rais. Ameahidi mengi kubwa ni kuboresha maisha ya wananchi wa Afrika Kusini. Kujua kama kweli Zuma anamaanisha anachosema, tumeweka hiyo picha ya makazi yake ya kifahari yaliyozamisha mamilioni ya rand huku jirani yake kukiwa na kibanda cha wale anaosema ataboresha maisha yao. Je kama alishindwa kufanya hivyo miaka mitano iliyopita ataweza kwenye kipindi hiki cha lala salama?Je ni yale yale ya Maisha Bora kwa Wote wote waliolengwa wakiwa ni familia na marafiki na waramba viatu wa rais? Hakika yetu macho kungoja kuona Zuma atakavyowakomboa au kuendelea kuwanyonya na kuwazamisha wananchi.