Kwa watu wanaojua jinsi rais Jakaya Kikwete asivyopenda kujisomea, wanashangaa anapopata uchungu na elimu. Japo hii inaweza kuonekana kama kumponda Kikwete, kwa wanaojua alivyoweza kuwakingia kifua mawaziri wake waliotuhumiwa kughushi elimu wanashangaa uchungu wa Kikwete kwa elimu. Kwa waliosahau ni kwamba Kikwete amewakingia kifua mawaziri Makongoro Mahanga, Mary Nagu na Wiliam Lukuvi na mawaziri wa zamani Emanuel Nchimbi, Deodorous Kamala aliyemteua balozi Ubelgiji. Je mtu wa namna hii anaweza kuwa na uchungu na elimu? Je hii gea ya kutoa vitabu jeshini inalenga kuonyesha nini? Je Kikwete anajiweka karibu na jeshi ili vitisho vyake na Lukuvi vionekane kuwa kweli? Ama kweli alichofanya Kikwete ni sawa na kile cha wahubiri uchwara na wanafiki katika Biblia ambao Yesu aliwakaripia waliokuwa wakiwahubiri watu kusikiliza wawahubiriyo bila kuangalia watendavyo.