Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175

Ridhiwani anataka kumdanganya nani?

$
0
0

Mwana wa rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani aliyepitishwa na chama cha baba yake kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze ametoa mpya kuwa akienda bungeni atawafundisha wabunge kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya kulalamikia posho za vikao.
Wengi wanjjiuliza: Kama Ridhiwani ana uchungu na taifa ni kwanini hakumuelimisha baba yake kuweka maslahi ya taifa mbele kwa kulinda raslimali za umma? Kama Ridhiwani ana uchungu na taifa hili,  kwanini hakujitenga na kutumia jina la baba yake kupata huo ubunge anaotaka kutumia kuwafundisha wakongwe kujali maslahi ya taifa ambayo yamehatarishwa na baba yake marafiki zake na familia yake? Je Ridhiwani anataka kumdanganya nani? Je Ridhiwani hajui na kuona kuwa anajidanganya kudhani atawadanganya watanzania kuwa ana uchungu na nchi wakati ni mmojawapo waliofika hapo walipo kwa kuihujumu hiyo nchi anayodai kuwa na uchungu nayo? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175