Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175

Mjue nshomile mwizi anayeita dola milioni 75 pesa ya ugoro.

$
0
0


Kwa wasiojua ujambazi wa wa IPTL ambao Tanzania imefanyiwa tangu mwaka 1995, nyuma yake kuna nshomile mmoja aitwaye James Rugemalira mmilki wa Mabibo Breweries. Mwizi huyu alitoa mpya juzi alipokaririwa akisema, "Niliiambia Serikali kuwa nyie mmeibiwa na sisi tumeibiwa. Mimi nikawaambia kuwa ‘the end justify the means’ (jambo la muhimu ni matokeo, si njia ulikopitia), mwisho tulikubaliana kwamba kwa masilahi ya Taifa tumalize kesi hii, na mimi ndiyo nikalipwa hivyo vijipesa vya ugoro."
Ashuukuru Mungu nchi inatawaliwa na wezi vinginevyo ingekuwa wakati wa mwalimu Nyerere angeozea gerezani. Ni ajabu kwa nchi inayokopakopa kuwa na mtu mwenye kuita bilioni 120 pesa ya ugoro. Je huyu jamaa ana ukwasi kiasi gani?
Wakati akijitapa, vyombo vya habari vimegundua kuwa kumbe yeye na washirika zake toka Malaysia wamekuwa wakilipwa dola 100,000 kwa siku kitapeli kwa kudai walikuwa na mtaji wa dola 50,000,000 wakati ukweli ni kwamba walikuwa na mtaji wa dola tano. Hata hivyo, ana hofu gani iwapo aliyekuwa waziri wakati wizi huu unafanyika sasa ni rais? Hata ukiangalia jina la kampuni ya mwizi huyu la VIP Engineering unapata swali moja kuu: Je kuna VIP nyuma ya wizi huu wanaompa kiburi huyu mwizi hadi kukufuru?

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175