Kuna utendaji, uwajibikaji na uadilifu hapa? Kweli kuna usoja mle au kiriba tumbo na magonjwa ya kila aina kuanzia ya kitabia hata ya kibaolojia. Je nchi zenye masoja kama hawa zimo kwenye hatari kubwa kiasi gani? Hilo wowowo ndiyo usiseme. Ikija kwenye friji wow! Only God knows! Ngai Muthamaki tuhonokye! Mnakumbuka jinsi masoja wa Kenya walivyokwenda kwenye Westgate or Wastegate mall kujiibia kila walichoweza huku wakisahau wajibu wao? Je Bongo mnao maafande wangapi mafisi na mafisadi wakubwa kiasi cha kuwalinda na kuwaengaenga mafisadi wakuu? Msijali. Nilikuwa nawaza tu baada ya kuona picha nzuri ya kupendeza kama hii. Tafakarini hata hivyo.