Wanaosema rais Jakaya Kikwete ni msanii hawakosei. Je hapa ana tofauti na marapper katika miziki ya kizazi kipya? Ukichanganya na "ujana" wake ambao ameu-maintain na kupata rangi nywele ili mvi zisionekane ndiyo usiseme. Nimependa staili yake ya kwenda na wakati ingawa si katika ofisi yake ambayo ameamua kuitelekeza akipendelea kusafiri ambao wabaya wake huita kuzurura.
Wakati ukututa ukifika hugota. Pamoja na jitihada zote, hapa uzee unaanza kujitokeza hata kama haukaribishwi. Mzee hapa hajapita saluni kupigwa soap soap aonekana kijana. Gaddafi alizoea hata kupiga wigi ili aonekana wamo wakati alikuwa kibabu!
Jamaa kwenye boxing yumo. Msanii lazima amudu sehemu zote. Hata kubembea ni sanaa. Au vipi?
Jamaa hajasahau vikwata wakati wa udogo wake.
