
Kiongozi wa mapinduzi yaliyoiingiza Mali kwenye mtafaruko wa kidini na kisiasa, Amadou Sanogo yuko korokoroni akikabiliwa na mashtaka ya mauaji. Sanogo afisa wa cheo cha kati jeshini asiyejulikana, aliishangaza dunia pale alipomwangusha rais wa zamani wa Mali Amadou Touman Toure. Sasa kibao kimemgeukia kama kilivyomgeukia mwenzie wa Guinea Moussa Dadis Camara. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.