
"Tunatumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yen na mtaihangaikia nchi na kuleata faida numbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi yenu manweza kuishi hapa na kazi yenu ni kushinga kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya, viongozi hawafai...mnapata faida gani?"Jakaya Kikwete akiwa nchini Poland alipowaponda wanaomponda.
Hiyo hapo ni nukuu ya rais Jakaye Kikwete ambaye anaonekana kukwera na baadhi ya blog kwa kuishambulia serikali yake bila kujua kuwa huo ndiyo ukweli. Ingawa si lengo la blog hii kuchambua malalamiko ya Kikwete, amesema uongo kudai kuwa watu wanashinda kwenye blog. Watu tuna kazi zetu na hatuandiki kwa vile hatuna kazi za kufanya. Tunaishi maisha ya kuheshimika na elimu ya kutosha. Hivyo kama Kikwete anadhani wengi wa wanaoandika ni watu wa vijiweni kama wale aliowatengeneza huko si wote. Wengine kuandika na kufundisha ndicho kibarua chetu.
Maswali mepesi, kwani viongozi si wabaya na nchi haina hali mbaya iwapo wachache wanawaibia wengi kipuuzi? Je Tanzania si balaa tokana na uongozi mbovu wa Kikwete uliojaa uzembe dhidi ya ufisadi ujambazi na uuzaji mihadarati?