Hakuna ubishi kuwa rais Jakaya Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais aliyehudhuria misiba na maziko mengi kuliko waliomtangulia. Kwa juu juu hili linaweza kuchukuliwa kuwa ni mapenzi na kuwajali watanzania. Kwa undani, rais anapaswa kutupiwa lawama za kuwa legelege kwenye kupambana na ujambazi, ufisadi, mihadarati na jinai nyingine zinaua watanzania wengi. Blog hii pamoja na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Sengondo Mvungi, inamtaka rais Kikwete aache kushabikia misiba. Badala yake awahakikishie watanzania ulinzi.
