Kikwete anapomteua balozi wa heshima Ahmed Issa pichani na mkewe Julin wakati mtu mwenyewe hata hajulikani. Je ni kujuana, ukuadi, uzembe na ukosefu wa umakini, dili au vipi? Sitashangaa nikisikia siku moja amemteua Mohamed Gire wa Richmond kuwa balozi wa heshima. Huenda hawa marafiki wa Balali wana dili watakalolifanikisha la lala salama ya Kikwete. Ni bahati mbaya kuwa bado Kikwete anakimbiza rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza duniani kuizunguka dunia bila kujali kuwa anaumiza walipa kodi. Hakika Kikwete hatakaa ajifunze ukiachia mbali kushabikia kuombaomba kunakomuwezesha kuzurura kila uchao.