Msomaji hebu angalia madudu haya ya wizi wa mchana unaofanywa na anayeitwa mheshimiwa wakati ni mwizi tu wa kawaida. Mbunge wa viti maalum Catherine Magige anatuhumiwa na kukiri kujipatia pesa kwa ajili ya kuwahonga wapiga kura ili wamchague kwenye uchaguzi ujao. Hii ni EPA ndogo ambapo pesa na dhamana ya umma inatumika kutafutia pesa ya kuusaka ubunge. Mchezo wa wabunge hasa wa kuteuliwa kuunda taasisi umeshika kasi kumbe ni janja na njia ya kuchumia pesa kwa ajili ya malengo machafu ya kisiasa. Kwa mbunge kama huyu anayejiuza kwenye makampuni na taasisi za umma akisaka ngawira anaweza kumwakilisha mlalahoi wa kawaida au kuutumia ubunge wake kujiunza kwa wawekezaji na kuwauza watanzania? Je kwa zao la viongozi kama hawa tutafika kweli? Je nini kifanyike kuepuka balaa hili la kitaifa? Tafakarini kwa makini. Maana nyinyi ndugu zenu hata vizazi vyenu ndiyo waathirika na waadhirika wakuu.