Quantcast
  • Login
    • Account
    • Sign Up
  • Home
    • About Us
    • Catalog
  • Search
  • Register RSS
  • Embed RSS
    • FAQ
    • Get Embed Code
    • Example: Default CSS
    • Example: Custom CSS
    • Example: Custom CSS per Embedding
  • Super RSS
    • Usage
    • View Latest
    • Create
  • Contact Us
    • Technical Support
    • Guest Posts/Articles
    • Report Violations
    • Google Warnings
    • Article Removal Requests
    • Channel Removal Requests
    • General Questions
    • DMCA Takedown Notice
  • RSSing>>
    • Collections:
    • RSSing
    • EDA
    • Intel
    • Mesothelioma
    • SAP
    • SEO
  • Latest
    • Articles
    • Channels
    • Super Channels
  • Popular
    • Articles
    • Pages
    • Channels
    • Super Channels
  • Top Rated
    • Articles
    • Pages
    • Channels
    • Super Channels
  • Trending
    • Articles
    • Pages
    • Channels
    • Super Channels
Switch Editions?
Cancel
Sharing:
Title:
URL:
Copy Share URL
English
RSSing>> Latest Popular Top Rated Trending
Channel: Free Thinking
NSFW?
Claim
0


X Mark channel Not-Safe-For-Work? cancel confirm NSFW Votes: (0 votes)
X Are you the publisher? Claim or contact us about this channel.
X 0
Showing article 1706 of 3178 in channel 8805252
Channel Details:
  • Title: Free Thinking
  • Channel Number: 8805252
  • Language:
  • Registered On: March 5, 2013, 12:54 am
  • Number of Articles: 3178
  • Latest Snapshot: June 1, 2025, 6:18 am
  • RSS URL: http://mpayukaji.blogspot.com/feeds/posts/default?alt=rss
  • Publisher: http://mpayukaji.blogspot.com/
  • Description: I Fear Nothing But Fear Itself
  • Catalog: //thinking1343.rssing.com/catalog.php?indx=8805252
Remove ADS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178
↧

Kijiwe chafunga kumuombea Lissu

September 12, 2017, 4:54 pm
≫ Next: Zetu ni Uhamiaji au uhamishaji, biashara au bi hasara?
≪ Previous: Magufuli anapaswa kusikiliza wimbo huu kwa makini
$
0
0
    Image result for photos of tundu lissu   Taarifa za kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa kamanda Tunduni Lissu zimesikitisha kijiwe. Baada ya kuzinyaka, kila mmoja alionyesha kusononeka huku tukilaani ujinga, upumbavu na unyama huu.
            Mijjinga anaingia akiwa anasonya na kutikisa kichwa kwa hasira, ngoa na uchungu. Tokana na ukweli kuwa tulikuwa tumeishapata breaking news toka radio mbao, tulijua wazi kilichokuwa kimechukiza na kumsikitisha. Baada ya kuamkua anasema “hivi nani ataishi milele tumuone lau mjanja kuliko wauaji na washamba wanaoanza kuhalalisha utekaji na uaji kayani? Ama kweli kiburi ni fimbo ya mpumbavu. Unamwaga damu ya mtu asiye na hatia halafu utegemee mafanikio? Kawadanganya nani wapumbavu na wauaji nyie msio na akili wala maono?”
            Kabla ya kuendelea Msomi Mkatatamaa anamfariji kwa kumpigapiga mgongoni.  Anasema “brother hili tukio la kushambuliwa kwa mwanakijiwe mwenzetu Tunduni Lissu hata kama huwa hashiriki kijiwe limetuhuzunisha na kutuchukiza hakuna mfano. Hawa wanahizaya waliojificha nyuma ya kinachoitwa wahalifu wasiojulika ni woga na washamba wasiojua maana ya kuvumiliana. Wanadhani wanaweza kutunyamazisha. Wanaweza kumuua Lissu lakini si mawazo yake. Akifa Lissu mmoja wanaibuka kumi. Hivyo, dhamira yao ovu haitafanikiwa.”
             “Usemayo ni ya kweli. Kwani alivofishwa Ntikila si alikuja huyu Tundu? Waweza ua Tundu lakini hatoliziba hili tundu linilosababishwa waja wanene hata kuweka maisha yao hatarini ati. Kwani hao walotaka kumua wataishi milele wakati kila kit ki wazi kuwa kul nafsi zalikatul maut yaani kula nasi itaonya mauti?” Mpemba anajibu kwa hasira huku wanakijiwe wakishangaa anavyotafuna kimanga kama wamanga wenyewe. Laiti kingekuwa kimombo huenda angekuwa mbali na hapa kijiweni.
            Kapende anakula mic “sikutegemea kuwa tungefika hapa na kuonekana kama kaya katili na ya hovyo kama zile zinazotawaliwa na maimla katili na mauaji. Hapa lazima kuwa na mkono wa mtu. Je SMG walotumia hawa wahalifu ilipatikana wapi? Hapa ndata lazima watoe maelezo inakuwajekuwaje wahalifu wanatesa mchana kweupe bila kuwanyang’anya silaha wakati rahis alishaagiza wawanyang’anye hizo silaha?”
            Kabla ya kuendelea Mgoshi Machungi anamnyang’anya mic “hii shambuio inashangaza sana.
Je seikai iichukua hatua gani pae Lissu aipotoa taiifa kuwa anafuatwa na wahalfu wanaotishia usaaama wake zaidi ya kunyamaza?  Je hapa kwei itazuia wachovu kusema mambo tena yasiyopendeza? Je hawa ndata waikuwa wanafanya kazi gani wakati tinajua kuwa wamekuwa wakimfuata mjengoni na kumkamata au ni kwa vile si wa chama chao?”
            “Chungi veve sema kweli kweli. Kwanini data napata guvu ya kamata yeye jengoni lakini hapana linda yeye kama hapana tatizo? Hii tisa sana” anachangia Kanji.
            Msomi Mkatatamaa aliyekuwa akisiliza na kutikisa kichwa kila mara anaamua kutia guu “Kanji umesaidia kujibu swali kubwa yaani nini wajibu wa lisirikali kwa usalama wa wapingaji. Linachoweza kukufanyia si jingine bali kukusweka ndani kwa kulalamikalalamika. Tujulize maswali mengine. Je waliomshambulia Liisu si wale waliomtishia kwa bunduki Mapepe Ninaye alipochunguza hujuma ya Bashit dhidi ya Klaudz? Je hawa wahalifu walipata wapi SMG na jeuri ya kufanya uhalifu mchana kweupe tena kwenye makao makuu ya kaya? Je kwenye nyumba za wahishiwa hakuna walinzi? I can’t understand this game really. Je wafe wangapi ndipo lisirikali listuke na kutimiza wajibu wake au kwa vile Liisu ni mpingaji? Wameshindwa kupambana na majambazi na mafisi yanaoiba mawe yetu kila uchao wanahangaika na wapingaji wanaowapa vipande vyao? Hawa wahalifu wanapaswa kusakwa, kama alivyosema rahis, wakamatwe na kujibu mashtaka haya ya uuaji na upumbavu.”
            Sofia Lion aka Kanungaembe anakula mic “kusema ukweli haya mambo yanatisha. Ni ukatili, upumbavu na unyama vya hali ya juu. Nadhani kama kaya tunapaswa kuangalia historia yetu na kuzingatia umuhimu wa amani. Sidhani kama hawa wanaotaka kunyamazisha au kutoa roho za wenzao wana nafasi katika kaya hii. Sidhani kama hawa wanaotumia njia za giza ni wenzetu au wanataka kutuchonganisha? Maana haiwezekani mja aeleze maoni yake auawe. Hawa wana nia mbaya na kaya yetu. Hivyo, nashauri mamlaka ziwashughulikie haraka kabla mambo hayajavuka mipaka.”
            Mheshimiwa Bwege aliyekuwa kimya muda wote anaamua kukamuua mic “ nimewasikilizeni sana kwa muda mrefu. Hivyo nisemacho si kipya bali kutia msisitizo. Kwanza, nakubaliana huu ni ubwege wa mwaka kufikiri kuua nafsi kutaondoa tatizo. Pili, nakubaliana kabisa kuwa hapa lazima uwepo mkono wa mtu. Swali muhimu ni: kwanini ndata walipotaarifiwa hawakuchukua hatua wakati wanasifika kwa kumsweka Tunduni ndani bila makosa mara kwa mara? Lazima tuelezwe tujue. Maana hii kaya ni yetu sote bila kujali nani ni nani ilmradi uwe raia halali wa kaya hiii iliyozoeleka kuitwa kisiwa cha amani ambacho sasa kinageuka kisiwa cha mauaji na unyamazishaji. Hatuwezi woe kuwa mabwege kama hao wanaotaka kuua wenzao. Lazima tuseme hapana. Hivyo ndiyo sivyo.  Mtatupeleka pababaya mshindwe kututoa huko. Kubomoa ni rahisi kuliko kujenga. Ni bwege pekee adhaniaye kubomoa ni sehemu ya kujenga.”
            Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shangingi jeupe. Sie kwa hasira tulidhani ni la mabashite watekaji na wauaji. Tukiwa tumeliweka kati si akatoka mshikaji wetu ambaye jina sitaji!
Chanzo Tanzania Daima J'tano kesho.
↧
Search

Remove ADS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178

Trending Articles


Girasoles para colorear

December 11, 2013, 4:06 am

mayabang Quotes, Torpe Quotes, tanga Quotes

March 26, 2013, 7:05 pm

Tagalog Quotes About Crush – Tagalog Love Quotes

August 29, 2013, 4:32 am

OFW quotes : Pinoy Tagalog Quotes

November 19, 2013, 5:32 am

Long Distance Relationship Tagalog Love Quotes

February 19, 2014, 1:59 am

Tagalog Quotes To Move on and More Love Love Love Quotes

June 14, 2014, 6:39 pm

5 Tagalog Relationship Rules

August 20, 2015, 12:26 am

Best Crush Tagalog Quotes And Sayings 2017

May 15, 2017, 6:03 pm

Re:Mutton Pies (lleechef)

March 1, 2015, 4:30 am

FORECLOSURE OF REAL ESTATE MORTGAGE

July 8, 2012, 6:30 am

Sapos para colorear

June 6, 2013, 7:16 am

tagalog love Quotes – Tiwala Quotes

July 22, 2013, 4:04 pm

Break up Quotes Tagalog Love Quote – Broken Hearted Quotes Tagalog

September 21, 2013, 4:30 pm

Patama Quotes : Tagalog Inspirational Quotes

January 16, 2014, 5:20 pm

Pamatay na Banat and Mga Patama Love Quotes

February 24, 2014, 4:20 am

Tagalog Long Distance Relationship Love Quotes

April 28, 2015, 5:23 am

BARKADA TAGALOG QUOTES

April 17, 2017, 7:24 pm

“BAHAY KUBO HUGOT”

February 17, 2021, 11:08 pm

Vimeo 10.7.0 by Vimeo.com, Inc.

March 20, 2024, 9:50 pm

Vimeo 10.7.1 by Vimeo.com, Inc.

April 10, 2024, 9:16 am

Search

  • RSSing>>
  • Latest
  • Popular
  • Top Rated
  • Trending
© 2025 //www.rssing.com