Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173

Leo Tumetimiza miaka 19 ya Ndoa

$
0
0


Kwa ndugu jamaa na marafiki, leo mimi na mke wangu Nesaa tumetimiza miaka 19 tangu tufunge ndoa. Katika kusherehekea siku hii  muhimu kwetu, pia huwa tunakumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa kwa shujaa wetu Nelson Mandela-ambaye kama angekuwa hai leo-angetimiza miaka 99. Tumefurahia keki na kadi tulizonunuliwa na watoto wetu kila mmoja akieleza anavyojihisi kuwa wazazi wake ukiachia mbali Nkwazi Jr na Nkuzi ambao hawajui kuandika. Kwetu ndoa si ndoana bali shule na pepo. Tunazidi kumshukuru na kumuomba Mungu aendelee kutupa na kutujalia amani upendo na utulivu tangu mwanzo wa safari yetu. Tunazidi kushukuru kuwa upendo wa kweli na wa ari si kiungo ambacho kiliwahi kupungua au kukosekana tangu mwanzo wa safari yetu. Si hayo tu, tunamshukuru Mungu kwa kutujalia wana na mabinti si haba ukiachia mbali furaha na kufaana visivyo vya kawaida. 



Viewing all articles
Browse latest Browse all 3173