$ 0 0 Wapendwa wasomaji wa blog hii nawaleteeni habari njema kuhusiana na rafiki yetu Masangu Matondo wa Nzuzullima ambaye amepotea ugani mwake yapata mwaka sasa. Nilishauliza hata kwa dada Yacinta kama ana clue ya alikokuwa jamaa huyu. Leo katika kupita ugani mwangu sehemu ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ndoa yangu nilikuta ujumbe wa pongezi toka kwa Masangu. Nilifurahi na kumjibu nikitaka nimfichue toka huko alikokuwa amezamia. Hivyo ndugu yetu Masangu yuko hai mzima na mwenye afya. Mengi atasema mwenyewe.