Kama kila mtu atafikiria kula mbona tutakulana kama inavyoendelea ambapo mfagiaji hudokoa kwenye eneo lake na rais humogola kila mahali. Je hawa wasio na meno wala uwezo wa kupanga kula kama vile watoto, wazee, wagonjwa na wenye matatizo mbali mbali watakuwa wageni wa nani katika nchi hii ya kulana, kuliwa, kutafunwa na kutafunana? Hata hivyo faraja ni kwamba hata hawa wanaojisifu kuwala wenzao nao wanaliwa na wengine watokao mataifa ya ughaibuni kama tulivyoshuhudia hivi karibuni walaji wetu wakiliwa na Obama.