Kwa utani na uoni wa karibu kibonzo hiki kinaweza kuchukuliwa kama utani, kina ukweli usiopingika. Hebu fikiri kwa mfano kitendo cha Richmond-Dowans kubatizwa na kuitwa Symbion Tanzania tena ikazinduliwa na Obama. Hebu fikiria majizi kama Rostam Aziz eti naye kuwa miongoni mwa 'mabilionea' wa Tanzania waliokutana na Obama. Kituko zaidi eti na wezi kama Dewji nao walikuwamo. Kweli kwenye msafara wa mamba kobe wamo.