Image may be NSFW.
Clik here to view.
Marehemu baba wa taifa Mwl Julius Nyerere alituachia amali lukuki. Aliwahi kusimulia kisa cha mke wa Kaisari na kutuhumiwa kwa uchafu. Nyerere alisema kuwa hata kama mke wa Kaisari hakuwa ametenda kosa, kujiruhusu kushukiwa tu kulitosha kumuondolea heshima. Jana tulimsikia Kikwete akijitetea yeye na famillia yake ambayo ni haki yake. Hata hivyo, utetezi wake haukuwa na mashiko wala malezo ya kujinasua na tuhuma. Leo anaweza kujiaminisha kuwa yu safi. Sijui kama kashfa ya EPA kama kweli itachimbuliwa itamuacha akiwa safi. Anaweza kumtetea mwanae Ridhiwan kuwa hana mawaa. Kama kashfa ya utwaliwaji wa Shirika la Uchukuzi Dar Es Salaam (UDA) itafumliwa vilivyo bila kulindana, sijui kama itamwacha akiwa safi. Alimtetea mkewe Salma kuwa hana mawaa. Right, kama shughuli za kampuni yake ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) zitapigwa kurunzi vilivyo hatabaki safi. Utawala wa kijambazi wa kifamilia haukuanzia wala kuishia kwa Kikwete. Unakwenda mbali hadi wakati wa Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa ambao kimsingi ndiyo waasisi wa mfumo chakavu na ovu unaotuhagaisha kwa sasa. Hata hivyo, kutokana na sura nilizoona kwenye baraza la mawaziri, uwezekano wa kulindana na kukingiana vifua ni mkubwa.
Clik here to view.

Ewe Jakaya Kikwete, unamdanganya nani?
Twayajua yako yote, tokea EPA zamani
Ulishapoteza kete, tulia uraiani
Kaa ukiomba Mungu, mlindane mafisadi
Ulizoea ubwete, kwa sasa uko kizani
Nafasi usiipate, kuzurura ghaibuni
Kama unalo lolote, ulofanya ofisini
Kwenda kuzura hovyo, nao washikaji zako
Nenda kwa wauza kete, walioshika mpini
Ulisimama kidete, kuwahami hadharani
Imeshakwisha fungate, waingia matatani
Madudu yako Jakaya mbona yanajulika?
Kujinusuru ufyate, utegemee hisani
Au vipi yakukute, malipo ni duniani,
Uchunguzi ufuate, mengi watayabaini
Omba Mungu mlindane, mafisadi CCM.