

Mmojawapo wa Guptas akiwa na Duduzane Jacob Zuma (pichani)
Baadhi ya maafisa wa serikali ya Afrika Kusini wamesimamishwa kazi ili kuchunguzwa baada ya kuruhusu ndege binafsi kutua kwenye kambi ya kijeshi kinyume cha sheria. Waliosababisha kashfa hii ni 'matajiri' wa kutia shaka wa kihindi wa familia ya Gupta ambayo licha ya kuwa na urafiki na rais Jacob Zuma, ni washirika wa kibiashara wa mwanae Duduzane.
Ndugu watatu wa familia ya Gupta wanaosemekana kuanza kutajirika Zuma alipoingia madarakani, walitua kwa ndege yao binafsi na kufanyia sherehe za harusi karibu na kambi hiyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria.Ushirika wa mtoto wa Zuma na urafiki wa baba yake na familia ya Gupta umeamsha tashwishi na shaka hata shuku nyingi nchini Afrika Kusini hasa baada ya familia hiyo kumtenga Zuma na ujumbe wa watu alioandamana nao kwenye ziara ya kiserikali nchini India. Si Afrika Kusini tu ambapo familia ya Gupta imetia shaka na doa. Kwenye ziara ya Zuma nchini India, watawala wa India walishangaa hadi kuwauliza baadhi ya wajumbe inakuwaje rais anaburuzwa na matapeli kiasi hiki. Kutua kwa ndege kwenye kambi ya kijeshi kumeacha maswali mengi hasa ikizingatiwa kuwa ilikuwa ikitoka nje ya nchi ikiwa na watu 200. Je ndege hii ilikuwa imepakia bidhaa haramu kama mihadarati au wahamiaji haramu? Je watu wa uhamiaji walikagua abiria na bidhaa zilizokuwamo kwenye ndege hiyo? Wachambuzi wengi wamekuja na hitimisho kuwa Afrika Kusini haipaswi kuaminiwa tena kwenye masuala ya usalama pamoja na kuwa na nguvu nyingi za kijeshi barani. Je Zuma ameendelea kujivua nguo kutokana na kuwa na historia ya ufisadi? Je ndege hii ililete biashara za Zuma au mwanae? Je maadui wa kimataifa wakiamua kutumia njia si watafanikiwa hasa kipindi hiki cha ugaidi? Maswali ni mengi kuliko majibu. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa na HAPA naHAPA.