Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3185

Buriani Kamukara

$
0
0

Japo sikkuwahi kukutana na marehemu Edson Kamukara, tulifahamiana na kuongea sana karibu kila wiki kabla hajahama toka gazeti la Tanzania Daiam. Ndiye aliyekuwa mhariri wangu katika gazeti la Tanzania akishughulika makala zangu mbili maarufu kama Kijiwe na Nyingine ambayo sijui waliipa jina gani.
Nikiwa najiandaa kulala nilipitia kwenye mitandao japo kujua kilichojiri nyumbani. Kama kawaida huwa nasoma habari za huko hasa ikizingatiwa kuwa wakiamka tunalala na tukiamka wanajiandaa kwenda kulala. Hivyo, taarifa ya kifo cha Kamukara kilichotokana na moto wa jiko la mchina zimenichanganya kwa jinsi nilivyomjua kijana huyu ambaye alikuwa anaonyesha kuwa na bright future. Nimeona madhara ya mgao na umeme usio na uhakika umaskini na ushenzi mwingine vinavyoandama nchi za kiafrika. Ni bahati nzuri kuwa ni leo tu nilikuwa napitia kwa mara ya mwisho kitabu changu kipya cha AFRICA REUNITE OR PERISH ambapo masuala kama haya nimeyaongelea kwa undani zaidi.
 Kama nilivyodokeza hapo juu, sikumjua kwa sura japo tulijuana sana.
Kamukara alikuwa kijana si muaminifu bali mkweli na mstaarabu. Nakumbuka malipo yangu yakichelewa au kupunjwa alikuwa halali hadi anapata ufumbuzi. Kama hakuwa anacho anachojua aliweza kusema bila kuficha.
Kwa majonzi naona siwezi kuendelea. Ama kweli wema hawadumu.
NENDA SALAMA MAREHEME EDSON KAMUKARA
Mungu aiweke pema peponi roho yako.
Aaamiiiiiiiiiiiiiiiiiiinaaaaaaaaaaaa

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3185

Trending Articles


Girasoles para colorear


UPDATE SC IDOL: TWO BECOME ONE


Pokemon para colorear


tagalog love Quotes – Tiwala Quotes


The business quotes | Inspirational and Motivational Quotes for you


Long Distance Relationship Tagalog Love Quotes


“Mali man na ikaw ay ibigin ko, akoy iibig padin sayo”


RE: Mutton Pies (frankie241)


Vimeo 10.7.0 by Vimeo.com, Inc.


Vimeo 10.7.1 by Vimeo.com, Inc.


5 Tagalog Relationship Rules


HOY PANGIT, MAGBAYAD KA!


Sapos para colorear


Smile Quotes


Patama lines and Tagalog Quotes Pinoy Sayings


Tropa Quotes


Re:Mutton Pies (lleechef)


Ka longiing longsem kaba skhem bad kaba khlain ka pynlong kein ia ka...


EASY COME, EASY GO


FORECLOSURE OF REAL ESTATE MORTGAGE