Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178

Mlevi kutangazwa mlevi bora

$
0
0


Baada ya kugundua mbinu mpya ya kuongeza ujiko ili kuendelea kuwaibia walevi baada ya kuchemsha, mlevi ameingia na sayansi mpya. Najua wengi wanauliza hii ni sayansi gani? Simple, unaongea na washikaji wako wenye NGO za kusaka ulaji kitapeli wakupe kitu kama tuzo nawe unawapa chochote kitu na mambo yanaishia hapo.
Unapata ujiko wako huku wasiojua ‘chess’ nzima wanaamini sifa unazopewa unazo hata kama huna.
Wajinga ndio waliwao au vipi? Isitoshe si kila ving’aravyo ni dhahabu au goride au gold kwa ndugu zangu wa Malawi na Zimbabwe.
Hivyo, mlevi nimeamua kuchonga na ndugu zangu pale kwa Joji Kichaka wanitafutie NGO ya kunipa ujiko kwa vile nchi ile inaaminika kwa kusaka pesa kwa njia zote halali na haramu.
Bibie Libe Mura-muula aka nshomile upo maeneo ya Washing tone?
Nashukuru sana kwa vile mliwezesha bi mkubwa nami kupata tuzo na nafasi ya kuja huko majuu kushangaa shangaa na kukagua akaunti zetu. Nawashauri muendelee kutafuta wengine wenye kutaka ulaji kwa sharti la kutupa tuzo za hili na lile hiki na kile hata kama ni usanii mtupu.
Baada ya kutumia sayansi hii adhimu ya nyuma ya pazia mlevi nategemea kupewa tuzo ya kuweza kuwa mlevi wa kwanza tena kapuku kuzunguka mabaa yote ulimwenguni nikinywa kama akina Bill Gates bila kumsahau bi mkubwa ambaye huwa anaandamana nami kufanya matanuzi na shopingo aka shopping.
Sina haya ya kuongeza deni la walevi ‘pointlessly.’
Naona yule anatikisa kichwa na kudhania mie ni hamnazo na mpenda sifa kama Dk. Ziro wa kwenye hekaya za Oz.
Yule naye anadhani hizi ni kamba ajue mkono unaenda kinywani ukiachia mbali ujiko usio na utata ninaopata. 
Tuliza majeshi bro au sisie kama si shosti.
Mwenzio ‘soon’ nitapewa tuzo nyingine Bab kubwa ya kutumia sana njuluku za walevi na kufanya wafanye kazi zaidi na kuchangia matanuzi yangu.
Eneo jingine ninalotegemea kuniletea maujiko hata tuzo na maandamano ya walevi na wavuta bangi kunipongeza ni kutokana na umahiri wa kuweza kutoa ahadi nyingi ya kuwapa ofa walevi kuliko kiongozi yeyote wa walevi aliyewahi kutokea.
Japo ahadi hizi hazina uhakika kama ni za kweli au kamba, weye yakuhusu nini haya? Wajinga ndiyo waliwao. Lazima nami niwafaidi au vipi? Kwani kuna ubaya gani kuwala watu ambao wako tayari kuliwa? Kuna tatizo gani kuwala watu wanaojirahisi na kujitia kimbele mbele kama wale mabinti wa shule za msingi aliosema mkuu kuwa wanamimba kutokana na kiherehere chao japo madai kama haya ni kashfa.
Hayo tuwaachie wenye mabinti waamue kama ni kumponda na kumchukia jamaa au kujifanya hamnazo wakampenda badala ya kumponda na kumkaripia asirudie ili liwe somo kwa walevi wengine wa maulaji.
Eneo jingine ambalo lina ujiko wa wazi wazi usio na pingamizi wala mizengwe ni  kutokana na kuandaa utaratibu wa walevi kupata mwongozo mpya wa jinsi ya kulewa na kupambana na ndata.
Hili halijawahi fanywa na kiongozi yeyote wa walevi. Hili ni sawa na kuandika Katiba mpya ya walevi ambapo anayefanya hivyo hupata ujiko na kuheshimika sana kwenye midani ya mibangi na ulevi. Hata hivyo, ‘this move's its risks.’ Ukiamua kuandaa mwongozo mpya kwa walevi uhakikishe huuchakachui wala kujiingiza kwenye malumbano ya mwelekeo gani ufuatwe.
Hapa ukifanya kama alivyofanya mchovu fulani kule Idodomya kwa kukandia mapendekezo ya tume yake, walevi wanakutokea na michupa ili wakutie ngeu.
Uzuri wangu ni kwamba nitatumia njuluku ya walevi kwenda au kutuma makuwadi wa kupokea tuzo yangu. Kwanza,  lazima nitumie ili walevi wachange zaidi.
Lazima kuwepo gharama kwenda kukusanya ujiko wangu toka kwa Wanigeria wangu wanaotaka niwapigie ndogo waje kayani kula bila kutoa jasho kama wale waliokamatwa Tabata wakijifanya kuhubiri dini wakati ni wezi wa kawaida.
Nategemea kupata tuzo nyingine kutokana na kulea vizuri.
Nimefanikiwa kuonyesha kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka na nyoka mtoto ni nyoka na nyoka mzee alikuwa mtoto au vipi? Hivyo, nimewezesha kitegemezi changu kuanza kuukaribia ukuu kwenye kanywaji baada ya kukubaliwa na walevi achukue nafasi yangu ya zamani kwenye bunge la kanywaji. 
Kidume ameonyesha umahiri wa kupiga kanywaji na kupuliza mibangi.
Kuhakikisha hili linafanikiwa, nilitumia raslimali zote za walevi kumpigia kampeni kitegemezi wakati wa harakati za kugombea kiti changu kwenye kijiwe cha walevi.
Kimsingi, tuzo yangu ni tofauti na tuzo nyingine. Kwani kwa kutambuliwa na mataifa ya nje jinsi anavyolewa kistaarabu bila uchoyo ni kielelezo cha ukarimu wangu kuwa nikipiga mma napiga na kila mmoja mwenye ubavu wake hata kufanya hivyo kama kunawaumiza wengine.
Nani anajali iwapo wajinga ndio waliwao? Kwani huwaruhusu walevi kila mtu ajinywee atakavyo bila kujali kama wengine, hasa wadogo, wamepata au wamekosa kanywaji.
Naona yule anakandia kwa kusema eti tuzo yenyewe ni kipande cha kioo.
‘Well and good dude.’ We kipande chako cha kioo kiko wapi?
Wenzio hawaoni unachokiona. Japo kipande cha kioo ni cha hovyo, wenzio wanaona ni tunu na lulu. Hakika wajinga ndio waliwao! 
CHANZO: NIPASHE April 19, 2014.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3178

Trending Articles


Girasoles para colorear


mayabang Quotes, Torpe Quotes, tanga Quotes


Tagalog Quotes About Crush – Tagalog Love Quotes


OFW quotes : Pinoy Tagalog Quotes


Long Distance Relationship Tagalog Love Quotes


Tagalog Quotes To Move on and More Love Love Love Quotes


5 Tagalog Relationship Rules


Best Crush Tagalog Quotes And Sayings 2017


Re:Mutton Pies (lleechef)


FORECLOSURE OF REAL ESTATE MORTGAGE


Sapos para colorear


tagalog love Quotes – Tiwala Quotes


Break up Quotes Tagalog Love Quote – Broken Hearted Quotes Tagalog


Patama Quotes : Tagalog Inspirational Quotes


Pamatay na Banat and Mga Patama Love Quotes


Tagalog Long Distance Relationship Love Quotes


BARKADA TAGALOG QUOTES


“BAHAY KUBO HUGOT”


Vimeo 10.7.0 by Vimeo.com, Inc.


Vimeo 10.7.1 by Vimeo.com, Inc.