Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3185

JE HUU NI MWANZO WA MWISHO WA KUBENEA

$
0
0

 Zanzibar24 on Twitter: "Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA ...Kwa wachambuzi na wataalamu wa siasa, kitendo cha mbunge wa Ubungo aliyemaliza muda wake Said Kubenea kutimkia Chama cha ACT-Wazelendo ni pigo kubwa kwake na chama chake kipya. Kubenea ambaye alipata umaarufu baada ya kumwagiwa tindikali, hana sifa yoyote ya siasa ukiachia mbali kuwa hana taaluma wala elimu yoyote japo ya msingi, anachofanya ni kujikaanga kwa mafuta yake kama samaki. Kwa tunaomjua na tuliofanya kazi naye, Kubenea si mwanasiasa bali msaka tonge sawa na wasaka tonge wengine. Ni mbabaishaji ambaye hana ithibati kimaadili wala kisiasa. Kwa wale watakaokumbuka andiko hili, watakuja sema kuwa nilisema kuwa alichofanya Kubenea si chochote wala lolote bali kuanzisha mwanzo wa mwisho wake kisiasa. Ama kweli, la kufa halisikii dawa. Na isitoshe, ujanja ujanja una sifa ya kujenga mbegu na chembe za maangamizi ndanimwe. Kubenea si mpinzani bali msaka tonge ambaye yuko tayari kuuza utu wake kwa lolote. Kama anadai ana makazi Kinondoni na ana ofisi Kinondoni, kwanini aligombea ubunge Ubungo? Si aseme amemkimbia profesa Benephace Jocob ukiachia mbali kutapatapa? Sioni tofauti ya Kubenea na akina Gwajima na wasasi wengine wa tonge na ngawira. Ukiachia mbali kutapatapata, Kubenea unasumbuliwa na ukafu ambao umemfanya amfuate maalim Seif Sharif Hamad. Kwanini Kubenea ameshindwa kung'amua kuwa Zitto Kabwe mwenye ACT-Wazalendo atawatumia yeye Seif na Bernard Membe kama ambayo CHADEMA waliwatumia akina Edward Lowassa na Fredrick Sumaye na kuwatema kama ganda la muwa? Ugwiji wake wa kufanya utafiti uko wapi hapa wakati anaingia mkenge mchana kweupe? Kubenea amesahau kuwa watanzania sasa wanajua kuwa umaarufu wake haukutokana na sifa wala umahiri bali kumwagiwa tindikali. Hivyo, alipata kura za kuonewa huruma ambazo kwa sasa hazitakuwapo. Je huu ni mwanzo wa mwisho wa Said Kubenea msaka tonge aliyepata umaarufu baada ya kumwagiwa tindikali?


Viewing all articles
Browse latest Browse all 3185

Trending Articles


Vimeo 10.7.1 by Vimeo.com, Inc.


UPDATE SC IDOL: TWO BECOME ONE


KASAMBAHAY BILL IN THE HOUSE


Girasoles para colorear


Presence Quotes – Positive Quotes


EASY COME, EASY GO


Love with Heart Breaking Quotes


Re:Mutton Pies (lleechef)


Ka longiing longsem kaba skhem bad kaba khlain ka pynlong kein ia ka...


Vimeo 10.7.0 by Vimeo.com, Inc.


FORECLOSURE OF REAL ESTATE MORTGAGE


FORTUITOUS EVENT


Pokemon para colorear


Sapos para colorear


Smile Quotes


Letting Go Quotes


Love Song lyrics that marks your Heart


RE: Mutton Pies (frankie241)


Hato lada ym dei namar ka jingpyrshah jong U JJM Nichols Roy (Bah Joy) ngin...


Long Distance Relationship Tagalog Love Quotes