Tarehe 5 Februari 2020; wana-CCM wanaadhimisha miaka 43 ya uhai wa Chama chao. Tunapofanya sherehe hizo, ni vema tujikumbushe kule tulikotoka, yaani safari nzima iliyotufikisha hapa tulipo; pamoja na matarajio ya baadaye.
Kuhusu suala la tulikotoka, kuna mambo muhimu kadhaa ya kuzingatia, ambayo ni pamoja na haya yafuatayo:
USHIND WA CCM KATIKA CHAGUZI MBALI MBALI.
USHIND WA CCM KATIKA CHAGUZI MBALI MBALI.
(i) Kwamba katika kipindi chote hiki; Chama cha Mapinduzi kimeendelea kuwa ni Chama Tawala , kutokana na kwamba kimekuwa kikipata ushindi mzuri katika chaguzi zote zilizofanyika, ikiwa ni chaguzi zilizifanyika ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa tulio nao. (ii) Lakini pia yafaa izingatiwe kwamba kulingana na takwimu za matokeo ya Chaguzi hizo; kiwango cha ushindi wetu ( ambacho ndio ushahidi wa kukubalika kwa Chama chetu kwa umma wa Tanzania), kimekuwa kikipanda, na kushuka. Kilipanda sana katika miaka kumi ya mwanzo baada ya kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa: Tukianzaia kwenye uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995, ushindi wa Chama chetu uliongezeka katika uchaguzi mkuu uliofuata wa mwaka 2000; na ushindi wetu wet uliongezeka zaidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Lakini baada ya hapo, kiwango cha ushindi, hasa katika uchaguzi wa Rais wa nchi, kilianza kushuka katika uchaguzi wa mwaka 2010, na kiliendelea kushuka katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015.
ITIKADI YA UJAMAA.
(iii) Kuhusu utekelezaji wa Itikadi ya CCM ya UJAMAA, yafaa Wana-CCM tuwe wawazi na wakweli, kwa kukiri kwamba tulishindwa. Kwani siasa ya Ujamaa sasa imebaki katika maandishi tu ya vitabu na baadhi ya nyaraka za CCM; hususa katika kitabu cha Azimio la Arusha lenyewe; lakini siyo katika utekelezaji.
Lakini yafaa pia sababu za kushindwa huko zielezwe wazi, kwamba kubwa zaidi ni kwamba tulijaribu “kujenga Ujamaa bila kuwa na Wajamaa wa kuujenga”.
Ufafanuzi wake ni kwamba, kama Azimio la Arusha lenyewe linavyosema katika ukurasa wa 4; kwamba “Ujamaa ni imani. Hauwezi kujijenga wenyewe. Hauna budi kujengwa na watu wanaoamin na kufuata kanuni zake”. Basi ukweli ni kwamba hatukuwa na watu wa aina hiyo (waliokuwa tayari kufuata Kanuni za Ujamaa). Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyotufanya tushindwe kutekeleza ile DHANA (theory) yasiasa ya Ujamaa.
(iv) Lakini yafaa bado tujipe moyo, kwamba MOYO WA UJAMAA (the Ujamaa spirit) uliojengeka miongoni mwa Watanzania kutokana na mafundisho mazuri ya Azimio la Arusha, tumebaki nao moyo huo hadi sasa; na unaendelea kuonekana dhahiri katika maisha ya kila siku ya Watanzania wa leo. Ipo mifano mingi ya kuthibiisha hilo.
Kwa mfano, Dhana ya siasa ya Ujamaaa inasema hivi: “Katika nchi ya Ujamaa kamili, hakuna unyonyaji. Mtu hamunyonyi mtu mwenzake; bali kila awezaye kufanya kazi, hufanya kazi”.
Eneo hilo la ‘dhana ya siasa ya Ujamaa’, limeendelea kutekelezwa vizuri hadi hii leo; kwani vijana wengi sana hii leo, wanajituma kufanya kazi halali, za aina mbali mbali, ambazo zinawapatia riziki kwa nguvu zao wenyewe. Hao ni pamoja na ‘Wamachinga’, kina ‘Mama Ntilie’; na vyama vingi vidogo vidogo vya ushirika, vinavyopewa mikopo na Halmashauri za Wilaya.
Lakini zaidi ya hayo, moyo wa Ujamaa, wa kuheshimiana kwa misingi ya usawa wa binadamu; pia unaonekana dhahiri katika maisha ya kila siku ya Watanzania. Kuna vikundi vingi vya watu katika jamii yetu, vilivyoundwa kwa hiari na watu husika wenyewe; vya kusaidiana katika maisha, nyakati za furaha na nyakati za shida. Ndiyo sababu kuna vyama vingi vya Ushirika vya ‘Saccos’ na ‘Vikoba’ vilivyounndwa na watu wenyewe, vya kusaidiana kiuchumi; na pia kuna vyama vingine vingi, hasa Vijijini, vya kusaidiana nyakati za shida, hususan vinapotokea vifo. Kule kwetu Ukerewe, vinaitwa ‘Luguyo”.
Hii yote ni mifano inayothibitisha kwamba, hata kama DHANA ya Ujamaa ya “kuishi pamoja na kufanya kazi pamoja kwa faida ya wote”, ilishindikana kutekelzwa; lakini MOYO WA UJAMAA uliojengwa na Azimio la Arusha, unaendelea kushamini miongoni mwa Watanzania.
TATIZO LA KUFUTWA KWA MIIKO YA UONGOZI.
Lakini kuna tatizo kubwa lililosababishwa na uamuzi maarufu uliofanyika Zanzibar mwezi Januari 1991, uliofanywa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ambao kwa bahati mbaya ulipotoshwa sana wakati ule, kwa madai kwamba, eti, uamuzi huo “uliua Azimio la Arusha”.
Kwa hakika, huo ulikuwa ni upotoshaji mkubwa; kwa sababu, uamuzi huo kamwe haukuua Azimio la Arusha. Hii ni kwa sababu, jambo pekee lililobadilishwa katika Azimio la Arusha na kikao hicho cha Zanzibar; ni jambo moja tu, ambalo ni ile ‘Sehemu ya Tano’ ya Aziio hilo peke yake, ambayo inayohusu “Miiko ya Uongozi”. Sehemu zake nyingine zote; yaani kuanzia Sehemu ya Kwanza hadi Sehemu ya Nne, na muhimu zaidi ni ile ‘Sehemu ya Tatu’ inayozunumzia suala la KUJITEGEMEA, (ambayo ndiyo sehemu kubwa zaidi kuliko zote katika kitabu cha Azimio la Arusha),hazikuguswa kabisa na Kikao hicho cha Zanzibar. Kwa hiyo, kudai kwamba “Azimio la Ausha liliuawa Zanzibar”, ni upotoshaji mkubwa. Yapasa tuachane nao.
TUZINGATIE MABADILIKO MAKUBWA YA SERA ZA UCHUMI.
(v) Ni muhimu vilevile kuzingatia kwamba uamuziwa kikao hicho cha Zanzibar, ulifuatiwa mara moja na uamuzi mwingine muhimu, wa kubadilisha sera zake za uchumi, ambapo mnamo mwezi Februari mwaka huo huo wa 1991, Chama kilitangaza “mwelekeo wa sera zake za Uchumi katika miaka ya Tisini”
Mwelekeo huo mpya wa sera zake za kiuchumi ndio ulioruhusu sekta binafsi iweze kushiriki kikamilifu katika kuendesha uchumi wan chi yetu; ambalo lilikuwa ni jambo jema; kwani kushirikisha sekta binafsi kulisaidia sana katika kuimarisha uchumi wa nchi yetu, hasa kwa upande wa upatikananji wa bidhaa mbali mbali zinazohitajika kwa matumizi ya kawaida ya watu.
MIIKO YA UONGOZI ILIWEKWA KWENYE SHERIA ZA NCHI.
(iv) Ni muhimu pia kuzingatia, kwamba, pamoja na kuvurugwa kwa suala la ‘Miiko ya Uongozi’ kulikofanywa na Kikao hicho cha Zanzibar cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM; Miiko ya Uongozi ilihamishiwa katika sheria za nchi, na kuongezewa makali yake, kwa kuwekewa adhabu kwa wale watakaovunja mashari ya sheria hiyo. Kwa hiyo Miiko ya Uongozi iliendelea kuwapo.
KUPOROMOKA KWA MAADILI MIONGONI MWA VIONGOZI.
(v) Katika tathmini yetu, yafaa pia tukiri kwamba kumekuwapo na tatizo la kuporomoka kwa maadili miongoni mwa Viongozi wetu. Nionavyo mimi, ni kwamba kuna sababu mbili kubwa ambazo zimechangia katika uporomokaji huu wa maadili miongoni mwa Viongozi wetu.
Ya kwanza, ni kusitishwa kwa mafunzo ya maadili, ambayo yalikuwa yakitolewa katika vyuo vya Chama vya Kivukoni College, pamoja na vyama vyake vingine sita vya kanda, vilivyokuwapo katika Mikoa mbali mbali.
Lakini ni vizuri kwa wanachama kufahamu sababu ya kuchukuliwa kwa hatua hiyo ya kufunga vyuo vya Chama wakati huo. Ni kwamba, hatua ya kufungwa kwa vyuo hivyo vya Chama , ilitokana na kuingia kwetu katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Tukio hilo kubwa la kisiasa, lilisababisha pia mabadiliko mengine makubwa kufanyika katika mwelekeo, pamoja na malengo ya kisiasa ya Chama chetu; ambayo sasa yalibadilika na kuwa ni ‘kutafuta ushindi katika chaguzi za viongozi wa Dola’.
Lakini ni vizuri kwa wanachama kufahamu sababu ya kuchukuliwa kwa hatua hiyo ya kufunga vyuo vya Chama wakati huo. Ni kwamba, hatua ya kufungwa kwa vyuo hivyo vya Chama , ilitokana na kuingia kwetu katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Tukio hilo kubwa la kisiasa, lilisababisha pia mabadiliko mengine makubwa kufanyika katika mwelekeo, pamoja na malengo ya kisiasa ya Chama chetu; ambayo sasa yalibadilika na kuwa ni ‘kutafuta ushindi katika chaguzi za viongozi wa Dola’.
Ndiyo sababu, hata Katiba ya CCM ilibadilishwa kwa kuwekewa kifungu kipya katika sehemu yake inayozungumzia malengo muhimu ya Chama. Kifungu hicho kipya ni kifungu cha 5, ambacho kiliweka lengo jipya kabisa, ambalo lilikuwa ni: “kushinda katika chaguzi za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Zanzibar, ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa”.
Ushindani huo ndio hasa uliosababisha kuwapo kwa tatizo linguine la RUSHWA katika uchaguzi; kwani wagombea walio wengi , hususan katika hatua ya kura za maoni za kutafuta mshindi atakayegombea kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi unaohusika, wakaanza kutumia mkakati wa kutoa rushwa kwa wapiga kura wao, kama njia ya kujitafutia ushindi.
Sababu ya pili ya kuchukuliwa kwa hatua ya kufungwa kwa vyuo vya Chama chetu vilivyokuwapo; pia ilitokana na kuingia kwa nchi yetu katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, mnamo mwaka 1992. Ni kwamba, baada tu ya kuingia katika mfumo huo wa vyama vingi vya siasa; ile ruzuku iliyokuwa inatolewa na Serikali kwa Chama kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo katika Vyuo vya Chama vya Kivukoni College, na katika vyuo vyake sita vya kanda vilivyokuwa katika Mikoa mbali mbali; ILISITISHWA.
Hali hii ya kutokuwapo kwa msaada wa fedha za mafunzo hayo ya maadili na uadilifu kwa viongozi, pia ilichangia katika kuporomoka kwa maadili ndani ya Chama, kwa sababu ilibidi sasa kila kiongozi alazimike kutumia akili zake mwenyewe tu, katika shughuli zake za uongozi. Na kama wasemavyo Waswahili, “akili ni nywele, kila mtu ana zake”.
Hali hii ya kutokuwapo kwa msaada wa fedha za mafunzo hayo ya maadili na uadilifu kwa viongozi, pia ilichangia katika kuporomoka kwa maadili ndani ya Chama, kwa sababu ilibidi sasa kila kiongozi alazimike kutumia akili zake mwenyewe tu, katika shughuli zake za uongozi. Na kama wasemavyo Waswahili, “akili ni nywele, kila mtu ana zake”.
Taswira ya jumla ya Chama cha Mapinduzi.Hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Chama cha Mapinduzi kilikuwa katika hali nzuri sana. Ndiyo sababu katika uchaguzi wa mwaka huo, Chama chetu kilijipatia ushindi mnono na wa kishindo kikubwa. Lakini mara baada ya hapo, taswira ya Chama cha Mapinduzi machoni pa wananchi walio wengi, ilianza kuathiriwa sana, na mambo yafuatayo:
(a) Migogoro iliyojitokeza kwa kasi miongoni mwa viongozi, hususan baina ya makundi yaliyokuwa yakizozana na kuhasimiana miongoni mwa Wabunge wa CCM.

(c) Kujipenyeza, tena kwa kasi kubwa, kwa wafanya biashara wasio waadilifu, katika baadhi ya Vikao muhimu vya Chama vinavyofanya maamuzi .
(d) Chama kupoteza sifa yake yake ya asili, ya kuwa ni Chama kinachojali wanyonge; na kwa hiyo kikabebeshwa mzigo wa kuitwa eti ni ‘chama cha matajiri’.
Lakini kwa hivi sasa, wanachama tunayo sababu ya kufarijika, kutokana na kwamba shutuma zote hizo sasa hazipo tena, kwani zimefutwa na kazi nzuri sana ya kujirekebishwa, iliyofanywa, na inaendelea kufanywa, na viongozi wa Chama waliopo sasa
Matarajio ya baadaye.
Kazi nzuri inayofanywa na viongozi waliopo sasa, imeleta matumaini mapya miongoni mwa wanachama walio wengi. Kwa hiyo matarajio ya baadaye yanapaswa kuwa mazuri.
Hata hivyo, yafaa ikumbukwe kwamba Chama cha Mapinduzi, ni Chama kikongwe, kwa maana ya kwamba kimekuwapo, na pia kimekuwa madarakani mfululizo, kwa miaka yote tangu nchi yetu ilipopata uhuru wake.
Jambo hili la ukongwe wa Chama chetu, lina faida zake, lakini pia lina hasara zake. Faida yake ni kwamba kwa sababu ya uzoefu wake huo wa miaka mingi, kina fursa kubwa ya kuendesha shughuli zake vizuri, na kwa hiyo kuendelea kupata ushindi katika chaguzi zijazo.
Lakini kwa upande mwingine, kuwapo huko kwa muda mrefu kunaweza kusababisha hatari kubwa. Hii ni kwa sababu ya kwamba, kutokana na hulka ya binadamu ilivyo, wakati mwingine watu wanaweza kutaka mabadiliko tu ya uongozi wa nchi, hata kama Chama kilichopo madarakani kinafanya vizuri kiasi gani.
Maana yake ni kwamba, watu wanaweza kuchoka tu kuendelea kuwa chini ya uongozi wa Chama kile kile, miaka nenda miaka rudi! Na hatari hiyo inakuwa ni kubwa zaidi pale ambapo matendo ya viongozi wake yatakapokuwa mabaya kiasi cha kuwaudhi watu.
Kwa ajili hiyo, Chama cha Mapinduzi hakina budi, hususan kupitia viongozi wake, kioneshe kwamba kinaweza kuleta mabadiliko yenye tija, yenye kuleta matumaini mapya miongoni mwa wananchi walio wengi. Kiongozi mpya wa Chama chetu na Serikali, Rais aliyetokana na CCM, Dr. John Pombe Magufuli, ameleta matumaini hayo mapya miongoni mwa wananchi walio wengi. Kwa hiyo matarajio ya baadaye ni mazuri, kwamba CCM itaendelea kupata ushindi na kushika Dola kwa kipindi kingine kirefu kijacho.
Kwa ajili hiyo, Chama cha Mapinduzi hakina budi, hususan kupitia viongozi wake, kioneshe kwamba kinaweza kuleta mabadiliko yenye tija, yenye kuleta matumaini mapya miongoni mwa wananchi walio wengi. Kiongozi mpya wa Chama chetu na Serikali, Rais aliyetokana na CCM, Dr. John Pombe Magufuli, ameleta matumaini hayo mapya miongoni mwa wananchi walio wengi. Kwa hiyo matarajio ya baadaye ni mazuri, kwamba CCM itaendelea kupata ushindi na kushika Dola kwa kipindi kingine kirefu kijacho.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Chanzo: Cde Msekwa Mwenye.