Mwezi ujao watanzania na dunia nzima wataadhimisha miaka 20 ya kifo cha baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hivyo, kila mtu, kwa namna aliyomfahamu mwalimu, anapata fursa ya kumdurusu kama sehemu ya kumbukumbu ya gwiji huyu wa ukombozi wa Afrika ambaye wengi wanamkumbuka na kumkosa hasa michango yake katika ukombozi wa nchi nyingi. Kwa vile komredi Msekwa ni mmoja wa wanafunzi na wafuasi wa kweli wa Mwalimu Nyerere, maandiko yake ni kama dirisha katika maisha ya Mwalimu ambayo si wengi wanayafahamu. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.