Quantcast
Channel: Free Thinking
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175

LAITI WOTE TUNGEIPENDA AFRIKA NA KUWAZA KAMA RAIS MAGUFULI!

$
0
0

Rais john Pombe Magufuli anaweza kuwa rais pekee wa Kiafrika aliyeamua kukataa kuaminishwa kuwa Afrika ni bara maskini. Naungana na msimamo huu kama nilivyouandikia kwenye vitabu vyangu vingi vya kiada kuwa kinachochelewesha bara la Afrika ni ile hali ya:-
Mosi, kuwa-defined, sina neno la kiswahili na watu wengine hasa wale walioitawala na wale wanaolenga kuinyonya na kuendelea kuiibia na kuidhalilisha,
Pili, ni ile hali ya kuaminishwa kuwa mwafrika hana uwezo wa kufikiri sawa na wengine, hivyo, hawezi kufanya kitu chochote bila msaada wa wafadhili ambao wengi wao ni weupe au wakoloni wetu wa zamani toka nchi ya magharibi,
Tatu, ni ile ya kubaguliwa kulhali na kuaminishwa kuwa mwafrika ni tegemezi wakati ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa Afrika haikuwahi kuishi kwa misaada kabla ya kuja kwa ukoloni ambao uliwezeshwa na dini na mawakala wake wengine.
Nne, ni ile hali ya Mwafrika kubaguliwa na kila kitu chake tokana na msigi mbovu uliojengwa na dini ambazo ziligeuza kila kitu cha kiafrika cha kishetani huku wakitukuza kila kilicho cha wenye dini husika.
Magufuli, kama kiongozi na Mwafrika, ameamua kuanzisha vuguvugu jipya la kimapinduzi kifikra kwa kutaka waafrika wakengeuke na kubadili msimamo na kuanza kujiona kama matajiri na wenye uwezo sawa na watu wengine. Kwa wale ambao tumejikita kwa muda mrefu kwenye dhana ya decolonisation au uhurishaji, hili ni jambo jema sana.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 3175